Prevent men’s violence against women

Aina za ukatili na unyanyasaji – Types of Abuse – Swahili

Unyanyasaji wa kimwili

Unyanyasaji wa kimwili hufanyika wakati mtu anapotumia nguvu za kimwili kushinikiza uwezo na utawala wake juu ya mtu mwingine. Inaweza kuanza polepole na kuongezeka kwa polepole baada ya muda. Mifano ya unyanyasaji wa kimwili:

Unyanyasaji wa kimwili hufanyika wakati mtu anapotumia nguvu za kimwili kushinikiza uwezo na utawala wake juu ya mtu mwingine. Inaweza kuanza polepole na kuongezeka kwa polepole baada ya muda. Mifano ya unyanyasaji wa kimwili:
• Kugonga, kupiga kofi, kupiga mateke, kuuma au kutema mate
• Kutupa vitu au kuharibu mali
• Kuwanyanyasa watoto au wanyama kipenzi
• Kumfungia mtu ndani au nje ya nyumba
• Unyanyasaji unaohusiana na mahari

Unyanyasaji wa kingono

Dhuluma ya kingono ni aina yoyote ya shughuli ya kingono ya kulazimishwa au isiohitajika. Mifano ya unyanyasaji wa kingono:

• Kumlazimisha mtu kufanya ngono au kufanya vitendo vya kingono bila kibali
• Mguso usiohitajika
• Kusababisha maumivu kwa kusudi wakati wa kufanya ngono
• Kulazimisha kufanya ngono bila kinga dhidi ya ujauzito na magonjwa ya zinaa
• Kusema matusi au vichekesho vinavyomdhalilisha mtu kingono

 

Unyanyasaji wa kihisia na maneno

Unyanyasaji wa kihisia na maneno hauachi kovu ya kimwili lakini huathiri afya ya akili na ustawi wa mtu. Mifano ya unyanyasaji wa kihisia na maneno:

• Kumlaumu mtu kwa matatizo yote katika uhusiano
• Kuitana majina, kupiga kelele au kumlinganisha mtu na wengine ili kudhalilisha kujithamini kwake
• Kumuabisha mtu hadharini kimakusudi
• Kutishia kujitoa uhai
• Kumfanya mtu ahisi ana makosa kwa kukataa kufanya ngono
• Kutitisha kufuta visa kwa kuripoti kwa mamlaka ya uhamiaji

 

Unyanyasaji wa kifedha

Unyanyasaji wa kifedha hufanyika wakati mkosaji anaposimamia kabisa akaunti za benki, na kumzuia mhadhiriwa dhidi ya kutumia pesa au kufanya kazi. Unyanyasaji wa kifedha unajumuisha:

• Kusimamia kabisa mambo ya kifedha
• Kuzuia ufikiaji wa akaunti za benki na kadi za mikopo
• Kutoa pesa kidogo au hata kutotoa pesa zozote kwa gharama za nyumbani
• Kuomba pesa kila wakati (kutoka kwa mke au familia yake)

Unyanyasaji wa kijamii

Unyanyasaji wa kijamii hufanyika wakati mkosaji anapomtenga mpenzi wake kuzuia familia na marafiki ili ashinikize uwezo na utawala wake. Mifano ya unyanyasaji wa kijamii:

• Kufuatilia simu, ujumbe, barua pepe na mifumo ya mitandao ya kijamii
• Kuamua ni marafiki gani na wanafamilia gani ambao mpenzi wake anaweza kuona
• Kukosoa familia na marafiki wa mpenzi wake
• Kuhamisha eneo lililotengwa ambapo ni vigumu kwa mpenzi wake kuwasiliana na familia na marafiki
• Kulazimisha mtu kuolewa kinyume na matakwa yake (ndoa ya lazima)

Unyanyasaji wa kiroho

Unyanyasaji wa kiroho hujumuisha kunyima au kutumia vibaya imani na desturi za kiroho ili kumtawala mtu mwingine. Mifano ya unyanyasaji wa kiroho:

• Kumzuia mtu kufuata deni lake
• Kumlazimisha mtu kufanya vitu kupinga imani ya dini lake
• Kudhihaki desturi au imani ya kidini ya mtu
• Kutumia dini kuhalalisha ukatili.

Kunyemelea

Kunyemelea hufanyika wakati mtu kwa kusudi anaendelea kumfuata mtu kupinga na matakwa yake. Kunyemelea humfanya mhadhiriwa kuhisi ni kama amepoteza utawala wa maisha yake. Mifano ya unyemeleaji:

• Kupiga simu au kutuma ujumbe mara kwa mara
• Kumfuata mtu nyumbani au kazini
• Kuacha barua na maua zisizohitajika
• Kufuatilia matumizi ya teknolojia ya mtu k.m. simu, barua pepe, mitandao ya kijamii

 

Unyanyasaji unaotegemea picha

Unyanyasaji unaotegemea picha hurejelea mtu anayeshiriki au kutishia kushiriki picha za siri bila kibali cha mtu kwenye picha. Hizi zinaweza kuwa:

• Kushiriki picha za kimapenzi
• Picha za uchi kamili au sehemu
• Picha zinazoonyesha vitendo vya ngono
• Picha za sehemu za siri za mtu
• Kuongeza uso wa mtu kwenye picha ya ponografia au ya ngono na kusambaza picha hizo.

Subscribe to our newsletter