Facts about White Ribbon Australia (kiswahili) – Swahili

Kuhusu White Ribbon Australia

White Ribbon ndio vuguvugu kubwa duniani la wanaume na wavulana wanaofanya kazi kukomesha ukatili wa wanaume kupinga wanawake na wasichana, kukuza usawa wa kijinsia na kuunda ndoto mpya ya uume.

White Ribbon Australia, kama sehemu ya vuguvugu hili la kimataifa, inataka wanawake wote nchini Australia kuishi kwa usalama, bila ukatil i na unyanyasaji. Tunalenga kuzuia kwa msingi: kukomesha ukatili kabla ya kuanza .

Kupitia elimu, kukuza ufahamu na kampeni bunifu , mipango ya kuzuia na ushirikiano, tunaangazia jukumu nzuri ambalo wanaume wanatekeleza katika kuzuia ukatili wa wanaume kupinga kwa wanawake na kuwaunga mkono ili kuwa sehemu ya mabadiliko haya ya jamii.

Ndoto Yetu
Taifa ambalo linawaheshimu wanawake, ambapo kila mwanamke anaishi kwa usalama, mbali na aina zote za unyanyasaji wa wanaume.

Lengo Letu
Kuwahusisha wanaume ili kufanya usalama wa wanawake kuwa suala la mwanaume pia.

Wanaume kuongea na wanaume wengine kuhusu ukalili dhidi ya wanawake ni kichocheo thabiti cha mabadiliko.

Ukatili dhidi ya wanawake

Ukatili dhidi ya wanawake na unyanyasaji kupinga kwa wanawake hufanyika katika jamii zote na haujazuiwa kwa utamaduni wowote hasa. Hufafanuliwa kama “kitendo chochote cha ukatili wa kijinsia ambacho husababisha, au kinaweza kusababisha, madhara ya kimwili, kingono au kisaikolojia au kuumia kwa wanawake” na Umoja wa Mataifa. Tabia ya unyanyasaji hujumuisha uwivu, umiliki, udhalilishaji na vitisho . Ukatili haustahili kukubalika.

Ukatili wa kinyumbani na familia ni aina moja ya ukatili dhidi ya wanawake na mara kwa mara hupewa lebo ya ‘suala la kibinafsi la familia’ badala ya suala la umma linalofanyika duniani. Ni muhimu kuongea ikiwa wewe au mtu unayemjua anapitia ukatili na unyanyasaji.

Mpenzi, jamaa, rafiki au hata mtu mgeni anaweza kuwa mkoasaji wa ukatili, ijapokuwa ukatili na unyanyasaji hufanyika sana kati ya mkosaji mwanaume ambaye anajulikana na mhadhiriwa mwanamke.

Aina za ukatili na unyanyasaji

Aina zote za ukatili na unyanyasaji hazikubaliki. Zinaweza kutofautiana kuanzia ukatili wa wazi hadi unyanayasaji uliojificha na tabia za kuwasimamia kabisa wengine.

Unyanyasaji wa kimwili, kingono na kunyemelea ni aina za ukatili ambazo zinaweza kuonekana . Unyanyasaji wa kihisia, maneno, kifedha, kijamii, kiroho na unaotegemea picha unaweza kuwa umejificha na unaweza kutoonekana na marafiki na wanafamilia.

Soma Zaidi

Mahali pa kupata msaada

Ikiwa yuko hatarini ya sasa hivi, pigia simu Polisi, nambari ya simu 000.

Ikiwa wewe au mtu unayemjua anapitia ukatili na unyanyasaji, kuna msaada unaopatikana. Piga simu kwa mmojawapo wa nambari hizi ikiwa una maswali au unahitaji ushauri.

1800RESPECT

1800 737 732

Laini ya simu ya masaa 24 ya kimataifa ya ushauri wa ukatili wa kigono, familia na kinyumbani kwa mtu yeyote wa Australia ambaye amepitia, au yuko kwenye hatari ya, ukatili wa familia, kinyumbani na kingono. Wakalimani wanapatikana kwa lugha kadhaa.

Piga simu bila malipo 1800 737 732.

Tembelea tovuti

Lifeline

131 114

Lifeline ni nambari ya kitaifa ambayo inaweza kukusaidia kuwasiliana na huduma za wakati wa matatizo katika Jimbo lako.

Mtu yeyote nchini Australia anayepitia matatizo ya kibinafsi au anayefikiria kuhusu kujitoa uhai anaweza kupiga simu kwa 13 11 14

Tembelea tovuti

Huduma ya Utafsiri na Ukalimani

131 450

Pata mutaftiri bila malipo wa mkalimani wa simu au wa uso kwa uso kwa lugha yako mwenyewe. mutaftiri wa papo hapo wa simu unapatikana masaa 24, kila siku ya mwaka, nambari ya simu 131 450.

 

Tembelea tovuti

Maelezo

White Ribbon ina maelezo mengi kwa lugha tofauti na habari kuhusu kuzuia ukatili dhidi ya wanawake. Tazama mtandaoni, pakua au chapisha.

 

Tafuta maelezo

Mzunguko wa ukatili

Mzunguko wa ukatili huangalia hali inayojirudia ya hatua za mkosaji . Nadharia ya mzunguko wa ukatili huonyesha jinsi tabia ya mkosaji inaweza kubadilika kwa haraka sana, na kuifanya iwe vigumu kwa mwanamke kuondoka. Wanawake wanaopitia ukatili wanaweza kutambua mzunguko huu.

 

Awamu ya 1: Kuleta hamaki

Hamaki kati ya watu katika uhusiano huanza kuongezeka. Ukatili wa maneno, kihisia, au kifedha hufanyika. Tabia za mnyanyasaji huongezeka na kufikia mahali ambapo zinazidi kabisa.

Awamu ya 2: Ugomvi mkali

Ukatili hufikia kilele na mnyanyasaji huhisi vizuri. Hisia hii inaweza kuwa mazoea. Mnyanyasaji anaweza kuamua kushughulikia hasira zake kwa njia hii pekee.

Awamu ya 3: Fungate

Wakati huu, mnyanyasaji huanza kuhisi aibu na kuahadi hatakuwa mkatili tena. Kisha anaweza kujaribu kuelezea ukatili kwa kulaumu mambo mengine kama vile pombe au shida kazini. Mhadhiriwa huchanganyikiwa na kuumia lakini anatulia pia kwa kuwa ukatili umeisha. Mhadhiriwa anaweza kufikia mnyanyasaji amebadilika na hakutakuwa na ukatili tena.

Subscribe to our newsletter